CHEKI JINSI MTOTO WA RAIS JK ALIVYOMCHANA MBUNGE WA UPINZANI LIVE SOMA ALICHOKISEMA LIVE..!!!
siasa sio mizengwe bali ni kuonyesha njia wapi tunakwenda,Mbatia amenifunza mambo mapya. Hii sasa ndo siasa ya bongo
***********************************
MBUNGE WA SINGIDA: TUNDU LISSU WA CHADEMA AFUNGUKA: "NILISHA- PIGWA NA KULALA SELO MARA TATU,..SOMA ZAIDI HAPA
Mbunge
wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Tundu Lissu akiwa na spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda.
MBUNGE
wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Tundu Lissu amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya
uwakilishi wake bungeni, ameshapigwa na polisi kisha kuwekwa mahabusu
mara tatu katika maeneo tofauti nchini kwa sababu ya harakati za
kisiasa.
Akizungumza na waandishi wa Global Publishers katika
chumba cha habari Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki
hii, Lissu alisema kujiingiza katika siasa, hasa katika nchi ambayo
haipo tayari kwa siasa za upinzani kama Tanzania, unapaswa kujitoa na
kuwa tayari kwa lolote.
“Mimi nina familia yangu, unadhani
wanangu wanapenda kumuona baba yao anaadhirika kwa kuchaniwa shati lake
na kubebwa msobe msobe? Unadhani mke wangu anapenda kuniona
ninadhalilika kwa kupigwa na askari polisi hadharani? Ila nimejitoa na
nipo tayari kuhakikisha mambo yanakwenda sawa, hizi ndizo faida za kuwa
mwanasiasa wa nchi hii,” alisema.
Lissu ambaye pia ni Mnadhimu
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema ‘mtiti’ wa kwanza kukutana
nao ilikuwa ni wakati wa vurugu za wananchi wa wilaya ya Tarime wakati
wa mgogoro wao na wawekezaji wa North Mara, mkoani Mara, uliosababishwa
na kuuawa kwa watu watatu na walinzi wa mgodi huo.
Lissu alitoa
maelezo hayo baada ya kutakiwa kutoa historia ya harakati zake kwa
kifupi na kama kuna usawa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
Alisema
wanasiasa wa upinzani wanachukuliwa kama maadui na ndiyo sababu kila
mara wamekuwa wakiwekewa vikwazo katika utekelezaji wa majukumu yao
tofauti na wale wa CCM.
“Inataka uthubutu mkubwa kufanya
harakati ambazo tunazifanya. Linapokuja suala la kuwatetea wananchi na
rasilimali za nchi, inabidi uachane na maono ya kujiangalia kibinafsi,
badala yako utazame wajibu wako kama mtetezi wa taifa,” alisema na
kuongeza:“Sidhani kama ni sahihi kuliacha suala la utetezi wa nchi yangu
kwa watu wengine. Pamoja na yote ninayofanya bado natembea barabani
bila woga, maana ukiogopa kufanyiwa kitu kwa sababu ya harakati,
hutaweza kutembea wala kufanya chochote, kwa hiyo siogopi.”
*************************************************************************
KAMA WATU WANAJUA KULINDA TAMADUNI ZA KIAFRIKA HUYU NI NAMBA MOJA... HUYU NDO MAMA WA RAIS WA MALAWI...CHEKI RAIS ALIVYO MTEMBELEA MAMA YAKE KIJIJINI..!
Rais wa Malawi alipomtembelea mama yake kijijini.. Tumjaji vipi huyu kiongozi ..!! Ni mpumbavu kutopajenga kwao..? Au ni mtendaji kazi muaminifu kwa taifa lake..??
*************************************************************************
MAKUNDI YA URAIS YAIVURUGA CCM, SOMA ZAIDI HAPA
Dar es Salaam. Makundi ya Urais wa 2015 yanaendelea kuivuruga CCM baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Mgana Msindai kuibuka na kusema atamburuta mahakamani Mwenyekiti mwenzake wa Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ asipomwomba radhi kwa kumchafua kwa kumwita mpuuzi.
Hata hivyo, Kasheku amesema Msindai anaweza kwenda mahakamani huku akisisitiza kwamba hawezi kumwomba radhi kwa kuwa anaamini kwamba alichofanya ni kinyume cha taratibu za chama na vikao.
Juzi, Kasheku alimponda Msindai mbele ya waandishi wa habari kwa kitendo chake cha kusema kuwa wenyeviti wa CCM wa mikoa yote ya Tanzania wanamuunga mkono, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika safari yake ya urais wa 2015 wakati wa sherehe ya mwaka mpya huko Monduli, Arusha.
Msindai alisema jana kuwa amemtaka Kasheku aitishe mkutano wa waandishi wa habari na kumwomba radhi. “Asipofanya hivyo ndani ya siku saba nitampeleka mahakamani,” alisema Msindai.
Msindai pia alikanusha kuwa aliwekwa kitimoto katika mkutano wa wenyeviti wa CCM wa mikoa uliofanyika Zanzibar.
Msindai aliyekuwa Mbunge wa Iramba Mashariki kwa miaka 15, alikiri kuwa alialikwa pamoja na wenyeviti wenzake sita katika sherehe ya mwaka mpya iliyoandaliwa na Lowassa huko Monduli.
Katika sherehe hizo, Lowassa alitangaza kuwa ameanza safari ya matumaini, kauli ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliitafsiri kama tangazo la kuwania urais mwaka 2015.
Msindai alikanusha kutangaza kuwa wenyeviti wote wa CCM wa mikoa wanamuunga mkono Lowassa wakati wa sherehe hiyo... “Mimi ni Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, lakini sikuwahi kuzungumza kuwa wenyeviti wote wanamuunga mkono Lowassa katika Uchaguzi Mkuu 2015... kikubwa tulichozungumza ni kumuunga mkono katika safari yake ya mafanikio katika kuendeleza elimu, maji, ujenzi wa zahanati.”
Msindai alisema wanamwangalia Lowassa kutokana na uwezo wake katika kusimamia mipango yake ya maendeleo na zaidi katika kupigania elimu pana kwa Watanzania.
“Alipokuwa Wizara ya Maji alichangia maji kupatikana Dar es Salaam na mikoani na maendeleo mengi, uwajibikaji kwenye jimbo lake na aendelee hivyo...hayo ndiyo tuliyomsifia. Nilizungumza haya na sitabadilika,” alisema Msindai, ambaye alisema haogopi kufukuzwa.
“Mimi si mpya ndani ya CCM kama ‘Msukuma’. Nina miaka zaidi ya 40, ninaelewa taratibu zote za chama za udiwani, ubunge na urais. Kama ni kampeni ni baada ya chama kumpitisha mtu na sisi tutamuunga mkono... hata mimi ninaweza kuwania urais,” alisema.
Siombi radhi
Kwa upande wake Kasheku alisema hamwombi radhi Msindai, kwani si wenyeviti wote wa CCM wanaomuunga mkono Lowassa katika safari yake aliyoiita ya matumaini.
“Siombi radhi na hata sasa hivi anaweza kushtaki, tulipokutana Zanzibar alitueleza kuwa alitoa kauli ya kuumuunga mkono Lowassa kimakosa na kusema alikuwa akimaanisha yeye na wenzake aliokwenda nao Monduli ndiyo wanamuunga mkono Lowassa,” alisema Kasheku.
Kasheku alifafanunua kuwa Msindani alisema kuwa wanahabari walikosea kumnukuu baada ya kuandika katika vyombo vya habari kuwa alisema wenyeviti wote wanamuunga mkono Lowassa.
Alisema baada ya Msindai kukiri jambo hilo, wenyeviti waliokuwa Zanzibar waliandaa tamko la pamoja na kuagiza lisomwe na Msindai mbele ya wanahabri katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Dar es Salaam.
“Katika huo mkutano ilitakiwa niwepo mimi (Kasheku), Msindai na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, ila cha ajabu mwenzetu (Msindai) alitukimbia na tulipomtafuta akasema yupo Singida, hivyo sisi tuliamua kutoa tamko lile,” alisema Kasheku.
Alisema kauli aliyoitoa Msindai ni kinyume na maagizo ya wenyeviti wote wa CCM, huku akimtaka kabla ya kwenda mahakamani, ahakikishe kuwa amewasilisha malalamiko yake ndani ya chama ili Kamati ya Maadili ya chama ikae na kutoa uamuzi.
“Hatuna ugomvi na Lowassa, tuna ugomvi na yeye aliyetuweka nyuma yake na kusema wote tunamuunga mkono Lowassa, nani alimwambia maneno hayo na ilikuwa katika kikao gani?,” alihoji Kasheku na kuongeza:
“Kama kuna watu wapo nyuma ya Lowassa au mtu yeyote ni siri yao, iweje yeye atulazimishe sisi kuwa nyuma yake kwa mgongo wa Mbunge wa Monduli”.
Mgeja amtetea Msindai
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja ambaye pia alikuwa Monduli, alimtetea Msindai akisema hakuwahi kuzungumzia suala la urais katika mkutano huo wa Monduli zaidi ya kumsifu Lowassa kwa mafanikio aliyoleta kwenye jimbo lake na maeneo mengine alipokuwa Waziri Mkuu.
Alisema hakuna dhambi kwa kumpenda mtu yeyote, wote wanaotoa kauli za kukanusha ni dalili za woga, wivu, kutokujiamini na inawezekana wana watu nyuma yao.
MWANANCHI
Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,James Lembeli.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Utata umeibuka kuhusu wabunge waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuwa wanahusika na biashara ya pembe za ndovu.
Wakati Ofisi ya Bunge ikidai kuwa ripoti hiyo haina majina ya wabunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli ameshikilia kuwa majina hayo ni sehemu ya ripoti hiyo ambayo baada ya kuwasilishwa, iliibua mjadala ambao ulisababisha mawaziri wanne kuong’oka.
Gazeti hili limedokezwa kuwa majina ya wabunge hao yalitajwa mbele ya kamati hiyo wakati ikichunguza jinsi Operesheni Tokomeza Ujangili ilivyotekelezwa, baada ya kuwapo kwa malalamiko ya vitendo vya ukatili na utesaji wa raia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao hawakuitwa mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kutokana na kwamba suala hilo halikuwa moja ya hadidu za rejea walizopewa kuzitafutia majawabu.
“Sisi tulimaliza kazi na kuikabidhi Ofisi ya Bunge, ni kweli majina hayo hayamo kwenye ripoti (iliyosomwa bungeni) lakini nilikuwa navyo kwenye viambatanisho na ushahidi wake,” alisema Lembeli jana.
Alipoulizwa sababu za kutokuweka majina ya wabunge hao katika taarifa iliyosomwa bungeni Desemba 20, mwaka jana, mbunge huyo wa Kahama alisema: “Hiyo haikuwa kazi yetu sisi tulikuwa na wajibu wa kueleza yaliyotokana na Operesheni Tokomeza tu, lakini hayo mengine yapo kwenye viambatanisho.”
Ripoti ya kamati ndogo iliweka bayana jinsi watu mbalimbali walivyoteswa na vyombo vya dola wakati wa operesheni hiyo na baada ya mjadala bungeni, Rais Jakaya Kikwete alitengua uteuzi wa mawaziri hao.
Mawaziri wanne walioachishwa ni pamoja na Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Dk Mathayo David (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).
Ofisa wa Bunge, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake alisema taarifa iliyowasilishwa bungeni siku hiyo haikutaja majina ya wabunge hao na kwamba hata kwenye Hansard (taarifa za Bunge), za siku ya mjadala huo suala hilo halimo.
“Wabunge ni kama walifanya makosa, baada ya mwenyekiti (Lembeli) kusema kwamba wabunge wanatajwa kwa ujangili, walipaswa kutumia kanuni maana zipo, kutaka majina yao yatajwe,” alisema ofisa huyo.
Kauli yake iliungwa mkono na Naibu Spika, Job Ndugai ambaye alisema: “Kimsingi kwa mujibu wa taratibu za Bunge, taarifa inayowasilishwa bungeni ndiyo inayosomwa na ni wazi kwa umma, haiwi siri.”
Ndugai alisema katika mazingira hayo, isingekuwa siri kama majina hayo yangetajwa kwenye taarifa ya kamati.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni